Jinsi Ya Kuongea Na Mwanamke Kwa Mara Ya Kwanza

Kuongea na mwanamke kwa mara ya kwanza ni rahisi. Unachohitaji ni mambo matatu tu. Kwanza ni kujiamini, pili ni kuwa na mistari, tatu nikufunga mchezo. Huu ndio mfumo ambao marafiki zako wengi wangeweza kukuambia pindi ambapo utawauliza jinsi ya kuongea na mwanamke.
Hapa Nesi Mapenzi tunaamini kuwa kuongea na mwanamke kuna hatua na mchakato ambao unauhitaji kuufuata bila kuruka hatua hata moja. Lengo letu ni kuhakikisha ya kuwa hakuna hatua itakupita. Tutakupatia zana zote ambazo unahitaji kuzifahamu ambazo zinahusiana na wanawake. Ok, je wazifahamu njia ya kutumia hadi uanze kuongea na mwanamke? Zama nasi. #1 Angalia usafi wako. Kabla hujachukua hatua yeyote ya kuongea na mwanamke hakikisha kuwa uko nadhifu. Kwanza piga mswaki, valia nguo safi na pia ukiwa na marashi jipulize. Hii itakusaidia kwa kuwa ukiwa mchafu basi hakuna mwanamke yeyote atakubali kuongea nawe. Pia hakikisha unapoamua kumuapproach unaangalia nguo ulizovalia. Je, nguo umevalia kinamna gani. Huwezi kuapproach mwanamke uongee naye katika klabu wakati umevalia kana kwamba unaenda kwa ibada. Hakikisha kuwa nguo zako unazozivaa zina wiana na mazingira ulipo. #2 Muapproach ukiwa anakuona. Wakati unamuapproach mwanamke huyu hakikisha tayari amekuona. Usimuapproach kama mwizi. Nenda moja kwa moja sehemu ambayo yuko huku ukionyesha tabasamu la kuwa uko tayari kuongea na yeye pindi ambapo utamfikia. #3 Miondoko ya mwili. Mwanamke kuongea ama kukataa kuongea na wewe kutategemea pakubwa na miondoko yako ya mwili. Ok, tayari umemuapproach huyu mwanamke. Je ni hatua gani unachukua? Ukianza kutokwa na kijasho ama kigugumizi cha ghafla ama kujikuna kichwa na kucheza na miguu basi fahamu miondoko yako ya mwili haifai na mwanamke atakupiga chenga wakati wowote. #4 Tabasamu. Kama nilivyotangulia kusema ya kuwa lazima uwe unatabasamu ukiwa unaaproach mwanamke, hivyo hivyo ni muhimu kutabasamu wakati umekaa kando ya mwanamke. Hii ni muhimu kwa kuwa utamfanya mwanamke huyu kujihisi huru mbele yako na pia ni njia moja wapo ya kujitokeza kirafiki. #5 Mwangalie machoni. Ushamfikia huyu mwanamke. Kitu ambacho kinafuatia ni lazima uonyeshe ujasiri. Na ujasiri wako utaonekana pale ambapo utamwangalia huyu mwanamke machoni. Ukiwa unaanza mazungumzo na yeye, haupaswi kuangalia upande ama kuangalia chini. #6 Tumia ishara za mikono. Kutumia mikono yako mara kwa mara kuashiria kitu ama jambo fulani kunakupa ujasiri wa ghafla. Pia matumizi ya ishara hizi husaidia kusisitiza jambo fulani kando na kuwa inakupatia utulivu wakati mazungumzo yenu yanaendelea. #3 Zingatia himaya yako. Himaya yako ni ile sehemu ambayo unakuwa umeimiliki wakati mnaongea. Ukiwa umejifinya kwa kuchukua nafasi ndogo zaidi basi mafanikio yako kwa huyu mwanamke pia huwa finyu. Mfano kama unaongea na huyu mwanamke mkiwa kati kochi, halafu wewe umejifinya kwa kujiweka mwisho kabisa na kuchukua nafasi kidogo basi mwanamke unayeongea naye atakuona muoga. Pia kwa kuwa wewe na huyu mwanamke mumekutana mara ya kwanza, hupaswi kujionyesha wewe ni wewe. Hivyo unachohitajika kufanya ni kuchukua nafasi tu ile ya kawaida wakati mnazungumza. #8 Tumia sauti na lugha inayofaa. Ukiongea kwa sauti kubwa na mwanamke basi utampa ishara ya kuwa wewe ni duko, yaani masikio yako ni mazito. Ukiongea haraka haraka atakuona wewe ni fala. Pia ukiongea kwa sauti laini atakuona wewe hujakomaa na hufanani na mwanaume thabiti. So hapa lazima ujifundishe jinsi ya kuongea na mwanamke vile inavyotakikana. Hali kadhalika, matumizi ya lugha yako ni muhimu. Usitumie lugha ya kudhalilisha mtu, usitumie matusi, usitumie lugha ya uchafu. Yaani hapa lazima uwe mstaarabu kwa kuwa ni mara ya kwanza kwako kuongea na huyu mwanamke. [Soma: Maneno matamu ambayo mwanamke angependa umwambie] #9 Msifu. Hapa Nesi Mapenzi huwa mara nyingi hatukosi kutoa point ya kumsifu mwanamke. Hii ni mbinu moja wapo ya kumfanya mwanamke ajiskie huru na kujiona kuwa angalau ameweza kumzuzua mwanaume. Kujipodoa lisaa lizima asubuhi hakuji hivi hivi! #10 Ingiza ucheshi ndani ya mazungumzo. Wakati unaendelea kuongea na mwanamke huyu, hakikisha ya kuwa unaingiza ucheshi ndani ya mazungumzo yako. Hii ni muhimu kwa kuwa wanawake huvutiwa na wanaume ambao ni wacheshi. #11 Jitoe katika mazungumzo kistadi. Ok, huwezi kuzungumza na mwanamke milele. Lazima itafikia wakati utahitajika kujitoa ili kuendelea na shughuli nyingine. Ukiona kuwa mazungumzo yenu yamefikia kiwango cha kuwa munaenda zaidi ya dakika moja bila mmoja wenu kuongea basi ni bora zaidi kujiondoa. Well, hizi ndizo hatua ambazo zinahitajika kuchukiliwa wakati ambapo unataka kuzungumza na mwanamke. Hakikisha kila moja ya hatua hizi unazichukua ili kufanikisha mpango mzima wa kufanikisha mazungumzo yenu. Halafu kabla sijasahau...usitoke hivi hivi bila kuchukua namba yake ya simu.

Comments

Popular posts from this blog

Ingiza Popote Bosi...

Jinsi Ya Kurespond Baada Ya Mwanamke Kukukataa

Faida Tano Muhimu za Wewe Kulala Bila nguo