Jinsi Ya Kutambua Iwapo Mwanamke Anakuchukia

Watu wengi ambao wanatutembelea inbox yetu mara nyingi wanakuwa na maswali ya kutaka kusaidiwa kumpata mwanamke wa ndoto yao. Utapata mmoja anakueleza kuwa amekuwa akimfukuzia mwanamke huyu kwa muda mrefu. Tatizo ni kuwa bado hajapata picha kwa nini hajafaulu. Mistari yuko sawa, sanaa ya kutongozea yuko sawa...yaani yuko sawa kwa kila kitu. Lakini tatizo linakuja pale ambapo mwanamke hatoi jibu sahihi. Mara anasema kesho mara kesho kutwa ama hajibu texts zako nk. Wengi wakija na tatizo kama hili tunawaelekeza watoe wanawake hao deti wakutane ili wazungumze ana kwa ana badala ya kutumia text. Na matokeo mara nyingi wanarudi na kusema kuwa wameona kuna hatua ambayo inaonyesha matumaini. Kwa bahati mbaya, kuna baadhi ambao wanarudi na kuanza mada ile ile ya kuwa mwanamke huyo bado hamuelewi. Well, tulikaa chini na paneli yetu ya Nesi Mapenzi tukajadiliana na tukaona ni vyema kuja na hoja ya kutambua iwapo mwanamke anakuchukia wakati unapomtongoza. Hii itapunguza wakati ambao utakuwa unamuapproach kwa kuwa ukiziona ishara za kuwa anakuchukia tu unaachana naye na unatafuta mwingine. Zama nasi. Jinsi ya kutambua kama mwanamke anakuchukia. #1 Hajibu texts zako Wanawake ni viumbe ambao wanapenda kuwasiliana. Wakitumiwa jumbe na yeyote basi kwa kawaida ni jukumu lao kuhakikisha ya kuwa wanajibu. Hii ni natural. Lakini ukiona kuwa hajibu texts ama jumbe zako, usimuamini akikwambia kuwa alikuwa amesahau ama alikuwa yuko busy. Kama unaona ya kuwa hajibu texts zako hio ni ishara ya haraka kukuonyesha ya kuwa hajapendezwa na wewe. Fahamu ya kuwa wale wanawake wagumu wakiwa wamekupenda basi hawatajizuia kureply texts zako. #2 Yuko busy kila wakati. Anaweza kuwa ni mkurugenzi wa kampuni flani ama labda ni meneja katika shirika tajika, lakini kila mwanamke anaweka malengo yake muhimu mbele. Ukimskia kuwa hawezi kuwa na time kwa sababu muda mwingi anakuwa busy, basi unapaswa kufahamu ya kuwa anakwambia maneno hayo kwa kuwa hataki kuspend time nyingi na wewe. #3 Hajitokezi kwa zile sehemu ambazo alikuwa amezoea kutembelea. Wanawake ni viumbe wa mazoea. Wanapenda kutembelea sehemu ambazo wamezoea kutembelea. Na ukiona haonekani sehemu hizo basi kuna kitu ambacho anajaribu kukifich. Well, wewe umekuwa ukitembelea hii sehemu na mara kwa mara umekuwa ukikutana na huyu mwanamke. Ulipoanza kumtongoza, alikupa namba yake, mkawa mnaongea lakini ghafla unaona ya kuwa zile sehemu ambazo alikuwa anatembelea haonekani tena...hii ni ishara tosha kuonyesha kuwa anakimbia kitu, na ni wewe mmoja wao. #4 Anatoka wakati wewe unajitokeza. Ukiwa unaingia sehemu flani, labda katika mkahawa. Halafu ghafla yule mwanamke uliekuwa unamtongoza anajitafutia kisababu anaondoka, then hapa atakuwa anajaribu kukulenga na hataki kukuambia moja kwa moja kuwa anaudhika na wewe. #5 Anakuambia ubaya wake. Mara nyingi, wanawake watakuambia ubaya wao kuwahusu. Anaweza kuambia anavuta sigara, yeye ni mlevi chakari, ama ni mvivu nk. Yaani ili mradi umuone ya kuwa ni mwanamke asiyekufaa. Ukiona mwanamke ambaye akiwa anazungumza na wewe anakuambia maovu yake, basi anakuambia ya kuwa uachane naye na utafute mwanamke mwingine ambaye ni bora zaidi kumliko. #6 Hataki kuwa na wewe faraghani. Hii ni ishara kubwa zaidi kuonyesha kuwa mwanamke huyu hakupendi. Ukiona ya kuwa mwanamke huyu anakwambia, “tukutane kule” ama hapendi kukutana na wewe faraghani, labda anakataa mwitiko wako wa yeye kukutembelea kwako basi hapo unapaswa kujua mwanamke kama huyu hana hisia na wewe kamwe. Kama ni mwanamke ambaye anakupenda ukimwita faraghani anaweza kukuambia sitoweza kuja sababu naogopa kuwa na wewe pekeetu. Lakini mwanamke ambaye hakupendi atakwambia wazi kuwa mimi siwezi kuja kwako ama atakuwa anakupa ahadi zisizotimia. So lazima uwe mjanja ukiona ana tabia kama hizi. #7 Hakuna kitu spesho ambacho anafanya mkikutana. Anaweza kuwa interested na wewe kama rafiki, lakini si kama mpenzi wake. So ukiona ya kuwa mwanamke huyu hajitahidi kujirembesha ama kujipodoa, then kuna uwezekano mkuu mwanamke huyu amekuingiza katika himaya ya urafiki/friendzone. #8 Anapenda kuongea kuhusu wanawake wengine. Kama mwanamke anakupenda, mara nyingi anataka atenshen yako yote iwe kwake. Na akiona ya kuwa unaongea kuhusu wanawake wengine basi anashikwa na wivu. Lakini huyu mwanamke ulienae ukiona anapenda kuongea kuhusu wanawake wengine na haswa kueleza mambo yao chanya, basi uwezekano mkubwa ni kuwa anakuchukulia kama rafiki tu. Na hakuoni kama mpenzi mtarajiwa. #9 Anapenda kuja na mtu mwingine. Ishara nyingine kuonyesha kuwa mwanamke hakupendi ni pale ambapo ukimuita mtoke deti badala ya kuja pekeake anakuja na marafiki zake. Wanawake hupenda kutembea na marafiki zao ili kuleta furaha kwa kila sehemu ambazo wanakuwa. So ukiona amekuja na marafiki zake atakuwa anajaribu kuhepa kuongea na wewe. Ama hataki kuongea vitu serious na wewe. #10 Hakutambulishi kwa marafiki ama familia yake. Mwanamke akikupenda basi kwa kawaida anapenda kukutambulisha kwa watu ambao anawajali katika maisha yake. Anaweza kukutambulisha kwa mamake ama kwa babake, hii ni kawaida. Lakini wewe tayari ushaamua kujitambulisha kwa wazazi wake angalau wakujue, lakini unaona huyu mwanamke haeleweki basi hapo kuna kizungumkuti. Ijapokuwa hii inaweza kuwa ni ishara ya kuwa mwanamke huyu anakutaka wewe pekeako, pia inaweza kuwa ni ishara ya kuwa huyu mwanamke hakupendi. #11 Hakurushii mistari ama kukugusa. Wanawake pia hutongoza. Anaweza kukutumia jumbe za mahaba hadi ukachanganyikiwa. Lakini ukiona kuwa hakuna hata siku moja mwanamke huyu amekwambia kuwa anakupenda basi kuna shida. Vile vile, mwanamke anayekupenda kwa kawaida ukiwa mnaongea anaweza kukutomasa. Lakini ukiona hakuna hata moja ya haya mawili katika huyu mwanamke, basi unajisumbua sababu hakuoni kama mpenzi. Well, hizi ni ishara muhimu lazima uzingatie. Usijisumbue kuteseka na mwanamke asiyekupenda. Ni haki yako kujua iwapo anakupenda au la. Ishara ndizo hizo tumekupa. Ukiona iwapo mwanamke ulienaye anaonyesha baadhi ya hizi tabia tulizoziorodhesha, basi epuka na mapema.

Comments

Popular posts from this blog

Ingiza Popote Bosi...

Jinsi Ya Kurespond Baada Ya Mwanamke Kukukataa

Faida Tano Muhimu za Wewe Kulala Bila nguo