Sababu zinazomfanya mwanamke akunyamazie


Wanawake ni viumbe ambao hawaeleweki kirahisi. Wanakuwa na tabia nyingi ambazo haziwezi kueleweka kirahisi. Unaweza kuwa unaishi na mwanamke kwa muda mrefu hadi ikafikia mahali ukahisi kuwa unamjua vizuri lakini akajeuka ghafla.

Kusistiza swala hili ni kuwa unaweza kumtongoza mwanamke kwa muda mrefu, ukaona anaingia box halafu mara siku moja anakuzima. Unashindwa kuelewa shida ni nini.

Well, mambo kama haya hutokea. Unachotakiwa kufanya nikutambua mambo ambayo yanaweza kumfanya mwanamke, akupuuzie, ama akuondoe katika maisha yako.

Leo tumekuja na ishara 3 kuu ambazo zinamfanya mwanamke kukunyamazia. Labda umemtongoza kwa muda halafu akakunyamazia.

1. Hajui kuwasialiana na wewe ili kupata kile kitu anachotaka kutoka kwako.

Wanawake wengi wanakuwa wachangamfu kuongea. Wanaweza kuongea siku nzima na yeyote. Pia wanaweza kuwaambia chochote kile wanachotaka. Lakini tatizo ni kuwa wakiingia katika mahusiano, wanaweza kuwanyamazia wapenzi wao kwa kuwa wanashindwa jinsi ya kuongea nao. Inaweza kuwa maongezi yanapotea kwa kuwa hawajazoea kujipataka katika maisha mapya ya mahusiano. So inaweza kufikia mahali wakakunyamazia kabisa.

Jambo la kufanya ili kuepuka hali kama hii ni kuhakikisha ya kuwa ukimwona mwanamke ama mpenzi wako anakunyamazia na hujui sababu zake, ni bora umuulize shida iko wapi. Pia kwa upande wako jaribu kuvivunja vizingiti vyako ili mwanamke huyu aweze kutangamana na kuongea na wewe kiurahisi.

2. Anaona kuwa haumsikikilizi.

Wanawake ni viumbe wa kusikilizwa. Wanapenda kuona watu wakiwasikiliza. Hivyo wakiona dalili ama ishara za kuwa wanapuuzwa, haswa kwa wapenzi wao, basi inafikia mahali wanaamua kunyamaza. Hali hii hutokea wakati ambapo unamkatiza usemi mara kwa mara ama wakati mnabishana unabadilisha mada na kadhalika. Hali hii itamfanya mwanamke kujiona kuwa hana usemi mbele yako hivyo kuamua kunyamaza.

Kuepuka hali kama hii ni kuhakikisha ya kuwa unajipatia nafasi ya kumsikiliza mpenzi wako. Pia hupaswi kumkatiza usemi mara kwa mara ama hubadilisha mada. Mwanamke ameumbwa kuongea, na mwanaume ameumbwa kusikiliza.

3.Hana maneno mazuri yeyote ya kukuambia.

Wakati mwingine mwanamke anaweza kukunyamazia kwa kuwa amechoshwa na tabia zako kiasi cha kuwa anashindwa kutamka maneno mazuri kwako. Labda anakuona humridhishi kama zamani. Labda kitambo ulikuwa unampeleka deti, ulikuwa unamnunulia zawadi na kumsapriz mara kwa mara. Lakini siku hizi anakuona unachat na wanawake ovyo, unakuja kuchelewa nyumbani ama unakuwa na tabia mbaya ambazo hazifai. Hii inaweza kuwa sababu ya kunyamaza kwa kuwa anaogopa kuongea na wewe kwa kuwa anaweza kukutamkia maneno machafu ambayo hutayapenda kamwe.

Well, hapa ukimwona anakuwa na tabia kama hizi unamuuliza tatizo liko wapi. Kama umejiona kuwa wewe mwenendo wako wa maisha umebadilika basi itakubidi ubadilike ili mpenzi wako aweze kuongea na wewe tena.

Ok. Haya ndio mambo makuu ambayo huweza kumfanya mpenzi wako kukunyamazia. Hatari hapa ni kupuuzia mambo haya. Iwapo mwanamke ataendelea kukunyamazia halafu wewe hutafuti suluhu la tatizo hilo, inaweza kufikia pahali pabaya kwa kuwa mwanamke kama huyu anaweza kuamua kujiondoa katika mahusiano ambayo hayana furaha yeyote kwake



Comments

Popular posts from this blog

Ingiza Popote Bosi...

Jinsi Ya Kurespond Baada Ya Mwanamke Kukukataa

Faida Tano Muhimu za Wewe Kulala Bila nguo