Makosa 7 Ya Kijinga Ambayo Wanaume Hufanya Katika Mahusiano
Ni vizuri kufundishana. Kuna mambo ambayo mtu anaweza kufanya pasi na kujua kuwa anafanya makosa. Ikija katika masuala ya mahusiano, wanaume wengine huchukulia kama mzaha. Wakishafaulu kutongoza na kumteka hisia mwanamke, wao hujisahau na kuanza kuishi nao kama mtu wa kawaida. Leo tumekuja na ujuzi wa kukuonyesha makosa ambayo unaweza kuwa unayafanya bila kujua kuwa yana athari. Kiufupi ni makosa ya kijinga ambayo yanaweza kuepukika kirahisi iwapo utayafuatilia. Hii ni muhimu kwa kuwa ukiachana na makosa haya basi unaweza kudumu katika mahusiano marefu na mpenzi wako zaidi. Zama nasi. #1 Kuwa dume-toto Hii ni tabia ya kuwa umeingia katika mahusiano na mwanamke lakini bado una tabia za kitoto. Hapa unakuwa na tabia ambazo hazina misimamo, unakuwa na hisia haraka na hujiamini. Kwa mfano uko na huyu mwanamke lakini kama kuna kitu kimefanyika wewe ndio wa kwanza kukimbia ama kulia. Wewe huna misimamo katika maisha, mara leo unasema hivi na kesho unabadilisha. Na pia hujiamini. Mwanam...